Available languages:
Matukio ya Mwaka - Umoja wa Mataifa 2017
22 Dec 2017 -  Mwaka 2017 ulishuhudia mabadiliko ya uongozi katika Umoja wa Mataifa pale Katibu Mkuu António Guterres alipoanza mhula wake wakati changamoto za kimataifa zikiongezeka. Janga la wakimbizi linalokuwa kwa kasi zaidi duniani nchini Myanmar liliibuka wakati tishio la njaa likishika kasi Yemen, Sudan Kusini, Nigeria, na Somalia. Ili kuzuia migogoro kabla haijatokea, Katibu Mkuu Guterres alizindua mfululizo wa mageuzi yaliyolenga upatanisho na kinga. Haya hujenga katika mafanikio yaliyopita, yakiwemo urithi wa kujivunia ulioachwa na Mahakama ya Umoja wa Mataifa ya uhalifu wa kimataifa kwa ajili ya iliyokuwa Yugoslavia, ambayo ilifunga milango yake baada ya kuunda upya mkakati wa dunia dhidi ya uhalifu wa kivita, uhalifu wa kibinadamu na mauaji ya kimbari. Umoja wa Mataifa unapokabiliana na chagamoto za dunia za usalama, sauti za watu wanaoathirika zinavuma zikiwa na kusudio kuu kwa ajili ya mustakabali wetu wa pamoja.
Recent Video On Demand