Available languages:
Katibu Mkuu Ujumbe wa Siku ya Kimataifa ya Demokrasia (15 Septemba 2019)
26 Aug 2019 -  Moyoni, demokrasia ni kuhusu watu. Inajengwa na ujumuishi, kutenda usawa na ushiriki na ni msingi muhimu kwa ujenzi wa amani, maendeleo endelevu na haki za binadamu.
Maadili na matakwa haya yasionekane tu kama ishara au maneno matupu. Lazima yadhihirike katika maisha ya watu.
Lakini bado Siku ya Kimataifa ya Demokrasia inafanyika katika wakati huu ambapo uaminifu uko chini na hofu iko juu.
Watu wanasikitishwa na kuongezeka kwa pengo la usawa na kuvurugwa na mabadiliko yanayojitokeza kutokana na utandawazi na teknolojia.
Wanaona migogoro ikiendelea bila kutatuliwa, dharura ya mabadiliko ya tabianchi ikiendelea bila kujibiwa, ukosefu wa haki unaendelea bila kushughulikiwa, na fursa za raia zikipungua.
Tunapoadhimisha Siku ya Demokrasia, ninazisihi serikali zote kuheshimu haki ya kushiriki kikamilifu; na ninawapongeza nyote ambao mnajitahidi bila kuchoka kuhakikisha haya yanafanyika.
Recent Video On Demand