Available languages:
KATIBU-MKUU -- UJUMBE WA VIDEO KWA AJILI YA SIKU YA WAKIMBIZI DUNIANI 20 Juni 2017
20 Jun 2017 -  Je, inakuwaje kukimbia vita, majanga au mateso?
Kuacha kila kitu?
Watu wengi kuliko wakati mwingine wowote wa maisha yetu, wanaishi na jinamizi hili.
Hadithi zao ni za kutia simanzi.
Shida. Kutengana. Kifo.
Nimekutana nao wengi ambao wamepoteza mengi sana.
Lakini hawakupoteza matumaini ya ndoto zao, kwa ajili ya watoto wao, au dhamira yao ya kuboresha ulimwengu wetu.
Na wanachokitaka ni ujira mdogo tu- msaada wetu wakati ambapo wanauhitaji zaidi.
Na mshikamano wetu.
Inahamasisha kuona nchi zisizo na kitu mara nyingi hujitoa zaidi kwa ajili ya wakimbizi.
Katika Siku ya Wakimbizi Duniani, tunatafakari ujasiri wa wale waliokimbia na ukarimu wa wale wanaowapokea..
Hebu tukamie kuanzisha tena uadilifu wa mpango wa kimataifa wa ulinzi kwa wakimbizi.
Na hebu tufanye kazi kumpa kila mtu fursa ya kujenga mustakhbali bora zaidi - kwa pamoja.
Asante.

The Secretary-General: World Refugee Day 2017