Available languages:
(Kiswahili) António Guterres (UN Secretary-General) - Message for The International Day of Peace 2018
21 Sep 2018 -  KATIBU MKUU -- UJUMBE KWA SIKU YA AMANI DUNIANI

21 Septemba 2018

Mwaka huu tunaadhimisha siku ya amani duniani, huku tukijiandaa kusherehekea maadhimisho ya miaka 70 ya Tamko la Haki za Binadamu duniani.

Nyaraka hii ya kimsingi inatukumbusha kuwa amani huimarika pale ambapo watu hawasumbiliwi na njaa, umaskini wala ukandamizaji, na hivyo kuwezeshwa kustawi na kufanikiwa.

Huku tukitumia Tamko la Haki za Binadamu duniani kama mwongozo wetu, ni lazima tuhakikishe tunatekeleza Malengo ya Maendeleo Endelevu.

Ninawahimiza mzungumze kwa uwazi. Kuhusu usawa wa kijinsia. Kuhusu jamii jumuishi. Kuhusu hatua dhidi ya mabadiliko ya tabia nchi.

Hakikisha unatekeleza haya yote iwe shuleni, kazini au nyumbani. Kila hatua ni muhimu.

Na hebu tuchukue hatua pamoja kukuza na kulinda haki za binadamu kwa wote, kwa lengo la kuwa na amani ya kudumu kwa wote.