Available languages:
Kumbukumbu ya mauaji ya Holocaust-António Guterres (Katibu Mkuu wa UN)
23 Jan 2018 -  Video ya ujumbe wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres katika Siku ya kumbukizi ya waathirika wa mauaji ya Holocaust.

Leo tunawakumbuka wayahudi millioni sita, wake kwa waume pamoja na watoto waliotokomea katika mauaji ya Holocaust. Wengine wengi pia walipoteza maisha yao katika ukatili huo ulioikumba dunia.
Hata hivyo miongo kadhaa baada vita vikuu ya pili ya dunia, tunashuhudia ongezeko la chuki dhidi ya Wayahudi pamoja na visa vingine vya chuki zisizo na sababu.
Makundi ya Unazi-maboleo pamoja na yenye misimamo ya upendeleo wa wazungu ni miongoni mwa vichocheo vya chuki kubwa.
Pia wakati mwingine maoni yasiyofaa yanajipenyeza katika jamii na ulingo wa siasa.
Ni sharti tusimame kidete dhidi ya kuhalalisha chuki kuwa kitu cha kawaida Wakati wowote ule na popote pale thamani za utu zinapopuuzwa sote tunakuwa mashakani.
Sote tunawajibu wa kupinga haraka ubaguzi wa rangi pamoja na ghasia.
Kupitia elimu na utangamano tunaweza kujenga mustakbali mwema kwa wote wenye kuheshimu haki za binadamu, utu na kuishi pamoja kwa amani.