Available languages:
Katibu mkuu ujumbe kwa ajili ya siku ya kimataifa ya amani (Septemba 21, mwaka 2019)
18 Sep 2019 -  Amani ipo katika kitovu cha kazi zetu zote katika Umoja wa Mataifa. Na tunajua kwamba amani ni zaidi ya ulimwengu usio na vita.
Inamaanisha jamii zilizo na mnepo na utulivu ambazo kila mtu anaweza kufurahia uhuru wa msingi na kufanikiwa badala ya kuhangaika kukidhi mahitaji ya kimsingi.
Leo amani inakabiliwa na hatari mpya: dharura ya hali ya mabadiliko ya tabianchi, ambayo inatishia usalama wetu na maisha yetu.
Ndio maana ni kaulimbiu ya Siku ya kimataifa ya amani mwaka huu.
Na ndio sababu ninafanya mkutano wa hatua kwa tabianchi.
Hili ni janga la kimataifa.
Ni kwa kufanya kazi kwa pamoja tu ndipo tunaweza kufanya maskani yetu ya pekee kuwa ya amani, mafanikio na salama kwetu na vizazi vijavyo.
Katika Siku hii ya kimataifa ya amani, nawasihi nyote:
Chukua hatua kwa tabianchi na kuzidai kutoka kwa viongozi wenu.
Haya ni mashindano ambayo tutaweza na ni lazima tushinde.
Open Video Category
Conferences/Summits