Available languages:
António Guterres (Katibu Mkuu wa UN) katika siku ya kimataifa ya Redio Duniani (13 Februari 2019)
11 Feb 2019 -  Ujumbe wa video wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres katika maadhimisho ya siku ya Redio Duniani (13 Februari 2019).
Redio ni chombo chenye nguvu.
Hata katika dunia ya sasa ya mawasiliano ya kidijitali, Redio inawafikia watu wengi zaidi ya chombo kingine chochote cha habari.
Inafikisha taarifa muhimu na kuelimisha kuhusu masuala muhimu.
Ni chombo kinachozungumza na mhusika moja kwa moja na kumshirikisha na watu wanaweza kutoa maoni yao, kueleza wasiwasi wao na malalamiko yao. Redio inaweza kujenga jamii.
Kwa Umoja wa Mataifa , hususan kwa operesheni zetu za ulinzi wa amani, Redio ni njia muhimu ya kufikisha taarifa, kuunganisha na kuwawezesha watu walioathirika na vita.
Katika siku hii ya Redio Duniani, hebu tutambue uwezo wa Redio katika kuchagiza majadiliano, uvumilivu na amani.
Asante.
Open Video Category
Conferences/Summits