Available languages:
KATIBU MKUU - UJUMBE KWA SIKU YA KIMATAIFA KWA AJILI YA WATU WENYE ULEMAVU - 3 Desemba 2019
3 Dec 2019 -  Tunapolinda haki za watu wenye ulemavu, tunasonga mbele kufikia ahadi kuu ya Ajenda ya 2030 - kutowaacha yeyote nyuma. Wakati bado tunayo mengi ya kufanya, tumeona maendeleo muhimu katika kujenga ulimwengu jumuishi kwa wote. Karibu nchi zote wanachama wa Umoja wa Mataifa zimeridhia Mkataba wa Haki za watu wenye Ulemavu na ninawahimiza wale ambao bado hawajafanya hivyo kuuridhia bila kuchelewa. Mnamo Juni, nilizindua Mkakati jumuishi wa wenye ulemavu wa Umoja wa Mataifa, ili kuinua viwango na utendaji kuhusu ujumuishaji wa watu wenye ulemavu, katika maeneo yote ya kazi yetu na ulimwenguni kote. Na kwa mara ya kwanza, Baraza la Usalama lilipitisha azimio lake la kwanza mahsusi kwa ajili ya ulinzi wa watu wenye ulemavu katika mizozo ya silaha. Tumeazimia kuongoza kwa mfano. Katika Siku hii ya Kimataifa, ninathibitisha tena azma ya Umoja wa Mataifa kufanya kazi na watu wenye ulemavu kujenga mustakabali endelevu, jumuishi na mustakabali wenye mabadiliko ambao kila mtu, wakiwemo wanawake, wanaume, wasichana na wavulana wenye ulemavu, wanaweza kufikia uwezo wao.
Open Video Category
Conferences/Summits