Available languages:
António Guterres (Katibu Mkuu wa UN) katika Siku ya Kimataifa ya kumbukizi ya waathirika wa mauaji ya Maangamizi Makuu (27 Januari 2020)
22 Jan 2020 -  Ujumbe wa video wa António Guterres, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, kwa Siku ya Kimataifa ya kumbukizi ya waathirika wa mauaji ya Maangamizi Makuu.
Katika siku hii tunakuja pamoja kukumbuka moja ya uhalifu mbaya zaidi katika wakati wetu: mauaji ya kupanga yaloyotekelezwa na manazi na washirika wao ya maangamizi makuu (Holocaust) ya Wayahudi milioni sita wanaume, wanawake na watoto na mamilioni wengine .
Tunaahidi kwamba asilani hatutosahau. Tunaapa kueleza hadithi zao na kuwaenzi kwa kutetea haki ya kila mtu ya kuishi kwa utu katika ulimwengu wenye haki na amani.
Miaka sabini na tano iliyopita, ukombozi wa kambi za kifo ulimaliza mauaji lakini uliushtua ulimwengu, kwani wigo kamili wa uhalifu wa Manazi umeonekana bayana.
Kutokana na matendo haya ya kutisha, Umoja wa Mataifa uliundwa kuleta mataifa pamoja kwa amani na ubinadamu wetu wa pamoja, na kuzuia kurudia kwa uhalifu kama huu dhidi ya ubinadamu.
Kuibuka tena kwa chuki katika miaka ya hivi karibuni, kutokana na machafuko ya itikadi kali kushambulia kwenye maeneo ya ibada, inaonyesha kwamba chuki dhidi ya Wayahudi, aina zingine za ubaguzi wa kidini, ubaguzi wa rangi na ubaguzi mwingine bado upo pamoja nasi.
Miaka sabini na tano baadaye, Unazi-mamboleo na fikra za kudhani wazungu ni bora zaidi zinaibuka tena, na kuna juhudi zonazoendelea kupunguza ukubwa wa mauaji ya maangamizi makuuna kuyakana au kudunisha jukumu la wahusika.
Lakini kama vile chuki inavyoendelea, vivyo hivyo linapaswa kuwa azimio letu la kupigana nayo.
Leo na kila siku, tunawakumbuka waathirika wa mauaji maya maangamizi makuu kwa kufuata ukweli, ukumbusho na elimu, na kwa kujenga amani na haki kote ulimwenguni.