Available languages:
António Guterres (Katibu Mkuu wa UM) Katika kumbukizi ya wahanga wa mauaji ya halaiki
26 Jan 2017 -  Video ya ujumbe wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres katika Siku ya kumbukizi ya wahanga wa mauaji ya halaiki
Leo tunakumbuka wahanga wa mauaji ya halaiki, janga kubwa kabisa katika historia ya binadamu.
Dunia ina wajibu wa kukumbuka kuwa mauaji ya halaika yaliyofanywa kwa kukapangwa kwa lengo la kutokomeza jamii ya wayahudi na wengine wengi.
Itakuwa kosa la hatari kubwa kudhani kuwa mauaji ya halaiki ni matokeo tu ya ujinga wa kundi la kihalifu la manazi. Ukweli ni kwamba mauaji ya halaiki yalikuwa ni kilele cha chuki, visingizio na ubaguzi dhidi ya wayahudi, jambo tunaloita sasa chuki dhidi ya wayahudi.
Cha kusikitisha na kinyume cha azma ya kutatua, chuki dhidi ya wayahudi inaendelea kushamiri. Tunashuhudia pia ongezeko la misimamo mikali, chuki dhidi ya wageni, ubaguzi wa rangi na chuki dhidi ya waislamu. Ukosefu wa fikra sahihi na stahmala vinarejea.
Hii ni kinyume kabisa na misingi ya maadili ya dunia yaliyomo kwenye katiba ya Umoja wa Mataifa na azimio la haki za binadamu duniani.
Kamwe hatuwezi kusalia kimya au kupuuza pindi binadamu wanapokumbwa na machungu.
Ni lazima tutetee walio hatarini na wakiukaji wa haki wafikishwe mbele ya sheria.
Na kama maudhui ya mwaka huu yanavyoelezea, mustakhbali bora unategemea elimu.
Baada ya machungu ya karne ya 20, hakupaswi kuwepo na fursa ya ukosefu wa stahmala karne ya 21. Mimi nawahakikishia kuwa kama Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nitakuwa mstari wa mbele kupiga vita chuki dhidi ya wayahudi na aina nyingine zote za chuki.
Hebu na tujenge mustakhbali wenye utu na usawa kwa wote- na tukumbuke wahanga wa mauaji ya halaiki ambao kamwe hatutaruhusu wasahaulike.