Available languages:
Ujumbe wa video wa Katibu Mkuu wa UN António Guterres na Mjumbe Maalum wa UN kwa Vijana Jayathma Wickramanayake kwa siku ya kimataifa ya vijana
10 Aug 2018 -  KM:
Nina Imani na uwezo wa vijana.
Amani, uwezo wa kiuchumi, haki ya kijamii, uvumilivu – yote haya na zaidi yanategemeana na kutumia uwezo walionao vijana. Si katika siku zijazo, bali leo. Sasa hivi.
Hii ndiyo maana ya siku ya kimataifa ya vijana.
Mjumbe wa Vijana:
Vijana duniani wanahitaji fursa salama ambapo wanaweza kutoa maoni yao kwa uhuru na uwazi, na pia kufuata ndota zao iwe kwenye maeneo ya umma, ya kiraia au kwenye mitandao.
Leo hii, zaidi ya vijana milioni 400 duniani wanaishi kwenye maeneo yaliyoathiriwa na vita au vurugu.
Mamilioni wengine wanakabiliwa na unyanyasaji, ukatili na wengine haki zao kukiukwa.
Miongoni mwa walio hatarini zaidi ni wasichana na vigori, kama ilivyo kwa wakimbizi na wahamiaji vijana, wanaoishi kwenye sehemu zenye migogoro, na jamii ya vijana wanaofanya mapenzi ya jinsia moja na wale waliobadilisha jinsia (LGTBQI).
KM:
Vijana wanahitaji elimu na kupewa fursa. Ajira bora. Ushiriki kikamilifu. Sauti na kushiriki kwenye majadiliano.
Nitahakikisha kwamba Umoja wa Mataifa unasikiliza sauti za vijana, unawawezesha na kufuata muongozo wao.
Septemba mwaka huu tutaanzisha mkakati mpya wa Umoja wa Mataifa kuhusu vijana, tukiongeza juhudi zetu za kuwafanyia kazi na kushirikiana nao.
Mjumbe wa Vijana na Katibu Mkuu ndani ya studio:
KM:
Kwa kuifanya Dunia kuwa salama kwa vijana, tunaifanya dunia iwe bora kwa wote.
Mjumbe wa Vijana: Heri ya siku ya kimataifa ya vijana!