Available languages:
António Guterres (Katibu Mkuu) katika kampeni ya mtandao wa kijamii wa Twitter kuhusu unyanyasaji na ukatili wa kingono
24 Sep 2019 -  Ujumbe wa video wa António Guterres, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, katika uongozi wa kampeni ya mtandao wa kijamii wa Twitter kuhusu unyanyasaji na ukatili wa kingono.
Kuzuia na kukomesha unyanyasaji na ukatili wa kingono unaofanywa na wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa ni kipaumbele cha juu.
Unahitaji ushirikiano wa viongozi wa ngazi ya juu wa Umoja wa Mataifa, asasi za kiraia na serikali.
Ndiyo maana nimeanzisha kikundi cha viongozi, kuonyesha azimio letu katika ngazi ya juu ya kisiasa ya kuzuia vitendo hivi na kuitikia haraka na kwa ufanisi yanapotokea.
Haki na heshima kwa waathirika ni kiini cha jitihada zetu.
Tumeimarisha mwitikio wetu.
Lakini mengi zaidi yanahitaji kutekelezwa.
Hebu niwe wazi: Bila ya ubaguzi, Umoja wa Mataifa kamwe hauna uvumilivu wa vitendo vya unyanyasaji na ukatili wa kingono.
Tutaendelea kufanya kazi kwa nguvu kuwapa haki waathirika na hatimaye kufikia lengo letu la pamoja la kuondokana na ukatili na unyanyasaji wa kingono.
Asante!
Open Video Category
Non-Governmental Organizations