Available languages:
UJUMBE WA KATIBU MKUU WA - KUMBUKIZI YA MIAKA KUMI YA TETEMEKO LA ARDHI HAITI
12 Jan 2020 -  UJUMBE WA KATIBU MKUU WA
KUMBUKIZI YA MIAKA KUMI YA TETEMEKO LA ARDHI HAITI

Siku hii, tunakumbuka mamia ya maelfu ya Wahaiti waliopoteza maisha na mamilioni walioathirika vibaya na tetemeko baya la ardhi lililopiga nchi hiyo miaka kumi iliyopita.
Tunawakumbuka pia wafanyakazi wenzetu mia moja na wawili wa Umoja wa Mataifa waliopoteza maisha siku hiyo.
Sitowahi kusahau pigo na huzuni iliyotanda kwenye Umoja wa Mataifa baada ya kutambua ukubwa wa janga hilo.
Moyo wangu uko pamoja na wale walipoteza familia, marafiki au wapendwa wao.
Katika kipindi cha muongo mmoja uliopita, Haiti imejijengea mnepo kupitia nguvu za watu wake na msaada wa mafariki zake wengi kuinuka tena kutoka kwenye janga hilo.
Kwa msaada wa jamii ya kimataifa, Haiti inajizatiti kufikia malengo ya maendeleo endelevu, ikiwemo kupitia kuimarisha taasisi ambazo ni muhimu kwa mustakabali na ustawi wa watu wake.
Kwa siku ya leo ninarejelea dhamira ya Umoja wa Mataifa kusaidia Haiti na watu wake kujenga mustakabali bora.
Open Video Category
Non-Governmental Organizations