Available languages:
António Guterres (Katibu Mkuu wa UN) Siku ya Chakula Duniani (16 Oktoba 2018)
11 Oct 2018 -  Baadhi ya watoto milioni 155 wana utapiamlo na wana uwezakano wa kuishi na athari za kudumaa maisha yao yote.
Njaa pia husababisha nusu ya vifo vya watoto wachanga ulimwenguni.
Hali hii haivumiliki.
Katika siku ya chakula duniani, hebu na tuahidi kuwa na dunia isiyo na njaa—dunia ambamo kila mtu ana pata mlo wenye afya na lishe bora.
Kutokomeza njaa kunamaanisha kuunganisha nguvu zetu.
Serikali na kampuni, taasisi na watu binafsi: Lazima tuunde mifumo endelevu ya chakula.
Leo hii, tunarudia upya ahadi yetu ya kuzingatia haki ya msingi ya kila mtu ya chakula na kutomwacha nyuma mtu yeyote.
Asante.
Open Video Category
Non-Governmental Organizations