Available languages:
Ujumbe Wa Katibu Mkuu Wa Un Kuwakumbuka Waliopoteza Maisha Wakati Wa Vita Kuu Ya Pili Ya Dunia
8 May 2020 -  Katika wakati huu wa ukumbusho na maridhiano, tunatoa heshima kwa mamilioni ya watu waliopoteza maisha katika Vita Kuu ya Pili ya Dunia, na kukumbuka kujitolea kwao.
Hatupaswi kusahau kamwe mauaji ya maangamizi makubwa na uhalifu mwingine mbaya uliotekelezwa na Manazi.
Ushindi dhidi ya ukandamizaji na udhalimu mnamo Mei 1945 ulikuwa mwanzo wa enzi mpya.
Uthamini wa mshikamano wa kimataifa na ubinadamu wetu wa pamoja vilisababisha kuzaliwa kwa Umoja wa Mataifa, na dhamira kuu ya kuokoa vizazi vilivyofuata dhidi ya janga la vita.
Ulimwengu wetu bado unateswa na athari za migogoro. Hata wakati wa janga la sasa ya COVID-19, tunaona juhudi mpya za kugawanya watu na kueneza chuki.
Tunapoadhimisha kumbukumbu ya miaka 75, hebu tukumbuke mafunzo ya mwaka 1945 na tushirikiane kumaliza janga na kujenga mustakabali wa amani, usalama na hadhi kwa wote.