Available languages:
António Guterres (Katibu Mkuu) ujumbe wa video wa siku ya afya duniani (7 Aprili 2020)
6 Apr 2020 -  Siku ya Afya Duniani mwaka huu inakuja wakati ambao ni mgumu kwetu sote.
Ujumbe wangu leo ni kwa wafanya kazi wetu wa hudumua za afya -wauguzi, wakunga, mafundi, wataalam, wafamasia, madaktari, madereva, wasafishaji, watawala na wengine wengi wanaofanya kazi mchana na usiku kulinda usalama wetu.
Leo tunashukuru sana kuliko wakati wowote kwenye nyote mnapofanyakazi usiku na mchana, mkijiweka hatarini kupambana na janga hili.
Mwaka 2020 ni mwaka wa kimataifa wa wauguzi na wakunga na ninataka kutambua utaalam wenu na kujitolea.
Sote tuna sababu ya kushukuru kwa huduma na utaalam wa wauguzi na wakunga . Natambua hivyo.
Wauguzi hubeba baadhi ya mizigo mkubwa kabisa ya huduma za afya.
Hufanya kazi ngumu na kwa saa nyingi, huku wakihatarisha kuumia, maambukizi na mzigo wa afya ya akili ambao unaambatana na kazi hiyo inayotia kiwewe. Mara nyingi hutoa faraja wakati wa mwisho wa maisha.
Wakunga hutoa faraja katika mwanzo wa maisha. Wakati wa janga kazi yao inakuwa ngumu zaidi, wakati wakileta watoto wetu wachanga katika ulimwengu huu.
Kwa wauguzi na wakunga wa dunia hii: Asanten kwa kazi yenu.
Katika nyakati hizi za kiwewe, nasema kwa wahudumu wote wa afya: tuko pamoja nanyi na tunawategemea.
Mnatufanya tujivunie, mnatuhamasisha. Tuna deni kwenu.
Asante kwa mabadiliko mnayoyafanya, kila siku na kila mahali.