Available languages:
Ujumbe Wa SG Kuhusu Haki Za Binadamu Na COVID-19
23 Apr 2020 -  Sisi sote tuko katika hili kwa pamoja: Haki za Binadamu na kupambana na COVID-19

Janga la COVID-19 ni dharura ya afya ya umma - lakini ni zaidi hivyo.

Ni janga la kiuchumi. Janga la kijamii. Na ni janga la kibinadamu ambalo lina hatari ya kuwa janga la haki za binadamu.

Mnamo mwezi Februari, nilizindua wito wa kuchukua hatua ili kuweka hadhi ya kibinadamu na ahadi ya Azimio la Haki za Binadamu katika msingi wa kazi yetu.

Kama nilivyosema wakati huo, haki za binadamu haziwezi kuwa za kutopewa kipaumbele katika nyakati za shida - na sasa tunakabiliwa na janga kubwa zaidi la kimataifa katika vizazi kadhaa.

Leo, ninatoa ripoti inayoangazia jinsi haki za binadamu zinavyoweza na lazima ziongoze majibu ya kupambana na COVID-19.

Ujumbe uko wazi: Watu - na haki zao - lazima viwe mbele na katikati.

Lenzi ya haki za binadamu inaweka kila mtu kwenye picha na inahakikisha kwamba hakuna mtu anayeachwa nyuma.

Majibu ya haki za binadamu yanaweza kusaidia kulipiga gonjwa la COVID-19, kwa kuweka umakini juu ya umuhimu wa huduma ya afya kwa kila mtu.

Lakini pia yanatumika kama mfumo muhimu wa onyo - unaoonesha ni nani anaathirika zaidi, kwa nini, na nini kifanyike juu yake.

Tumeona jinsi virusi havibagui, lakini athari zake zinabagua – kuweka wazi udhaifu mkubwa katika utoaji wa huduma za umma na kutokuwepo kwa usawa wa muundo ambao unazuia ufikiaji wa huduma hizo. Lazima tuhakikishe haya yanashughulikiwa vizuri katika majibu.

Tunaona athari kubwa zaidi kwa jamii fulani, kuongezeka kwa kauli za chuki, kulengwa kwa vikundi vilivyo katika mazingira hatarishi, na hatari za hatua kali za usalama zinazodhoofisha mwitikio wa kiafya.

Pamoja na kuongezeka kwa utaifa wa kujitenga, udikteta na harakati dhidi ya haki za binadamu katika nchi zingine, janga linaweza kutoa kisingizio cha kuchukua hatua za kukandamiza kwa sababu zisizohusiana na janga hili.

Hii haikubaliki

Zaidi kuliko wakati mwingine wowote, serikali lazima ziwe na uwazi, zenye kuchukua hatua na zinazowajibika. Raia na uhuru wa vyombo vya habari ni muhimu. Mashirika ya asasi za kiraia na sekta binafsi wana majukumu muhimu ya kutekeleza.

Na katika yote tunayofanya, hebu na tusisahau kamwe: Tishio ni virusi, sio watu.

Lazima tuhakikishe kuwa hatua zozote za dharura - pamoja na hali ya dharura - ni za kisheria, zenye uwiano, muhimu na sio za kibaguzi, zinalenga jambo na muda mahususi, na kuchukua njia zinazofaa kulinda afya ya umma.

Jibu bora ni lile ambalo hujibu sawasawa vitisho vya haraka wakati unalinda haki za binadamu na utawala wa sheria.

Kuangalia mbele, tunahitaji kujiimarisha vizuri. Malengo ya Maendeleo Endelevu - ambayo yametekelezwa na haki za binadamu - yanatoa mfumo wa uchumi unaojumuisha na jamii endelevu.

Kuimarisha uchumi na haki za jamii inaimarisha ustahilivu wa muda mrefu.

Kurejea katika hali nzuri pia lazima kuheshimu haki za vizazi vijavyo, kuongeza hatua ya mabadiliko ya tabianchi inayolenga kudhibiti hewa ya ukaa ifikapo mwaka 2050 na kulinda bianuwai.

Sote tumo katika hili pamoja.

Virusi vinatishia kila mtu. Haki za binadamu humwinua kila mmoja.

Kwa kuheshimu haki za binadamu katika wakati huu wa janga, tutaunda suluhisho bora na la pamoja kwa dharura ya leo na kupona kwa kesho.

Asanteni.