Available languages:
Hatua madhubuti kwa utu wa pamoja
6 May 2016 -  Mkutano wa dunia wa masuala ya kibinadamu ni nini?

Dunia iko katika wakati muhimu. Tunashuhudia kiwango kikubwa cha madhila kwa binadamu tangu vita vya pili vya dunia.Na hii ndiyo sababy ya kwa mara ya kwanza katika miaka 70 ya historia ya Umoja wa Mataifa, Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-moon ameitisha mkutano wa dunia wa masuala ya kibinadamu.

Hapo 23-24 Mai 2016, viongozi wa dunia watakutana Istanbul kwa ajili ya utu wa pamoja na kuchukua hatua kuzuia na kupunguza madhila kwa binadamu

Dunia itakuja pamoja kuahidi na kutangaza hatua za kijasiri katika kusaidia majukumu matano ya ajenda utu.

1. Kuzuia na kumaliza mizozo
2. Kuheshimu sheria za vita
3. Hakuna mtu wa kuachwa nyuma
4. Kufanya kazi tofauti kukidhi mahitaji
5. Kuwekeza katika ubinadamu

Kufahamu zaidi kuhusu tukio hili la kihistoria
http://www.worldhumanitariansummit.org

Taarifa kuhusu video hii
Imetolewa na Idara ya Umoja wa Mataifa ya Mawasiliano kwa Umma
Picha za ziada kwa ridhaa ya UNICEF na UNHCR

#ShareHumanity : #Utuwapamoja
Recent Video On Demand