Available languages:
Matukio ya mwaka 2016
23 Dec 2016 -  2016 – Mwaka ulioshuhudia matukio ya kutia moyo na kukatisha tamaa. Mkataba wa mabadiliko ya tabianchi ukitiwa saini na kuanza kutekelezwa, huku mizozo na majanga vikiendelea kukatili maisha ya watu kuanzia Afrika hadi Mashariki ya Kati. Vikundi vya wapiganaji vikipambana dhidi ya serikali, Umoja wa Mataifa nao ukijizatiti kuleta amani. 2016, watendaji wakuu wa Umoja wa Mataifa wakikabidhiana madaraka baada ya mmoja kumaliza awamu na mwingine akipokea kijiti huku akipigia chepuo mshikamano baina ya watu wote ili dunia iwe pahala pema pa ustawi kwa watu wote.
Recent Video On Demand