Available languages:
António Guterres (Katibu Mkuu) ujumbe wa video wa Siku ya Kimataifa ya Nelson Mandela 2020
13 Jul 2020 -  Kila Mwaka, kwenye siku ya kuzaliwa kwa Nelson Mandela, tunatoa heshima kwake kama mtetezi wa ulimwengu kwa usawa, utu na mshikamano.
Madiba alikua kielelezo cha maadili kwa karne ya 20, ambaye urithi wake usiokoma unaendelea kutuongoza hata leo.
Kauli mbiu ya Siku ya Kimataifa ya Nelson Mandela ni “Chukua hatua, hamasisha mabadiliko”.
Inaangazia umuhimu wa kufanya kazi kwa pamoja, kutoka serikali hadi raia, kujenga dunia yenye amani, endelevu na yenye usawa.
Tunaadhimisha siku hii wakati ambapo tishio la janga la COVID-19 linahatarisha kila mtu, kila mahali, na hususani walio hatarini zaidi.
Kwa kukabiliwa na changamoto hizi, viongozi ulimwenguni wanahitaji kutambua umuhimu wa umoja na mshikamano.
COVID-19 imeibua ukosefu wa usawa wa kupindukia.
Tunahitaji kupigana na janga hili la ukosefu wa usawa kupitia mkataba mpya wa kijamii kwa enzi mpya.
Kwa pamoja tu tunaweza kulishinda tishio tililonalo la COVID-19 na kusimama upya.
Wakati Umoja wa Mataifa unaadhimisha kumbukumbu ya miaka 75 wakati huu dhaifu, tunatafakari juu ya maisha na kazi ya Nelson Mandela, ambaye aliheshimu maadili ya Umoja wa Mataifa na ambaye alichukua hatua na kuhamasisha mabadiliko.
Licha ya kuwa mfungwa wa dhamira kwa miaka mingi, Madiba aliboresha utu wake na kujitolea kwa maoni yake.
Mfano wake uzingatiwe na serikali yeyote ile inayoweka wafungwa wa aina hiyo iwaachie.
Hatupaswi kuwa na wafungwa wa dhamira katika karne ya 21.
Nelson Mandela alitukumbusha kwamba: “Kadiri umaskini, ukosefu wa haki na ukosefu wa usawa ukiendelea ulimwenguni, hakuna yeyote anayeweza kupumzika kweli.”
Katika Siku hii ya Mandela, tukumbuke kuwa tunaweza, na lazima kuwa sehemu ya mustakabali bora, fursa na ustawi kwa watu wote kwenye sayari yetu imara.