Available languages:
Katibu Mkuu -- Ujumbe Wa Siku Ya Utu Wa Kibinadamu Duniani
18 Aug 2020 -  Katika siku ya mahitaji na utu wa kibinadamu Duniani tunaheshimu kazi za wadau wa mahitaji na utu wa kibinaadamu ambao wamezishinda changamoto kubwa za kuokoa na kuboresha maisha ya mamilioni ya watu.

Mashujaa hawa wa kweli wanafanya mambo ya kushangaza katika nyakati za kushangaza kusaidia wanawake, wanaume na watoto ambao maisha yao yanakatizwa na majanga.

Mwaka huu, wafanyakazi wa utu na mahitaji ya kibinadamu wamekuwa mstari wa mbele kuliko wakati wowote.

Wanashughulika kutatua janga la kidunia la COVID-19, na kwa hivyo kuongezeka kwa uhitaji mkubwa wa mahitaji ya kibinadamu kutokana na kuzuka kwa janga hili.

Kupoteza kazi/ajira, elimu, chakula, maji na usalama kunawapelekea mamilioni zaidi kukwama. Vizuizi vya safari kupunguza kasi ya kuenea kwa virusi inamaanisha kuwa jamii, asasi za kiraia na asasi za kawaida za ndani kama kawaida ndio watatuzi wa kwanza.

Mwaka huu, tunawasherehekea: watu ambao mara nyingi wana uhitaji wao wenyewe, kama jamii zinazowasaidia na kuwakaribisha wakimbizi, wafanyakazi wa afya ambao hujali wagonjwa na chanjo ya watoto, na wafanyakazi wa utu na mahitaji ya kibinadamu ambao hujadili maridhiano juu ya maeneo ya migogoro kutoa chakula, maji na dawa. Ni mashujaa ambao hawazungumziwi katika makabiliano dhidi ya janga na mara nyingi wao huhatarisha maisha yao ili kuokoa maisha ya wengine.

Leo, ungana nami katika kutoa shukrani zetu na kuwaunga mkono watu wenye uerevu/ujasiri wa kibinadamu, wahudumu wa afya na wakabilianaji wa kwanza ambao wanaonesha mshikamano na ubinadamu katika kipindi hiki tunacho wahitaji kuliko wakati wowote.
Recent Video On Demand