Available languages:
"Tahadhari kwa Dunia"- Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres, Ujumbe wa video
31 Dec 2017 -  Wapendwa marafiki kote duniani
Heri ya Mwaka Mpya
Nilipokabidhiwa ofisi mwaka mmoja uliopita, nilitoa ombi mwaka 2017 uwe wa amani
Kwa bahati mbaya – kwa namna mbalimbali hali imeenda kinyume
Katika siku ya mwaka mpya 2018, sitatoa ombi, nitatoa angalizo – angalizo la hatari kwa dunia yetu
Machafuko yamezidi kuongezeka na hatari mpya zimezuka
Hamasa ya dunia kuhusu silaha za nyukliaimefikia kiwango cha juu zaidi tangu wakati wa vitabaridi.
Mabadiliko ya Tabianchi yanaenda kasi kuliko sisi
Ukosefu wa usawa unaongezeka
Tunaona ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu
Utaifa na ubaguzi nao unaongezeka
Tunapoanza mwaka 2018 , natoa wito wa kuwa na Umoja
Ninaamini tunaweza kuifanya dunia yetu kuwa mahala salama na pa amani zaidi
Tunaweza kutatua migogoro, kushinda chuki na kutetea maadili ya pamoja.
Lakini tunaweza kufanya haya tu kwa pamoja
Nawaomba viongozi kila mahali kulifanya azimio la mwaka mpya:
Tupunguze mapengo. Kuondoa mgawanyiko. Turudishe uaminifu kwa kuwaleta watu pamoja tukiwa na lengo moja
Umoja ndio njia
Musthakbali wetu unategemea hili
Nawatakia amani na afya njema kwa mwaka 2018. Asante Shokran. Xie Xie. Merci. Spasiba. Gracias. Obrigado.
Recent Video On Demand