Available languages:
António Guterres (Katibu Mkuu) ujumbe wa video siku ya wanawake duniani 2021
5 Mar 2021 -  Janga la COVID-19 limefuta maendeleo ya miongo kuelekea usawa wa jinsia
Kuanzia kufutika kwa ajira hadi mlipuko wa kazi ya malezi isiyo na ujira, kuanzia kuvurugwa kwa shule hadi ongezeko la janga la ukatili majumbani na unyanyasaji, maisha ya wanawake yamepinduka, haki zao zimemomonyoka.
Akina mama, hususan wasio na wenza, wamekumbwa na kiwewe kikubwa na machungu,
Madhara yake yatadumu hata baada ya janga.
Lakini wanawake nao pia wamekuwa mstari wa mbele kwenye hatua dhidi ya hili janga.
Wamekuwa wafanyakazi muhimu wakiendelea kutunza wagonjwa, wakishikilia pamoja uchumi, jamii na familia.
Wao ni miongoni mwa viongozi ambao wameweka viwango vya ugonjwa chini na nchi kuwa kwenye mwelekeo wa kujikwamua.
Siku ya wanawake duniani mwaka huu inaangazia nguvu ya mabadiliko itokanaoy na ushiriki sawa wa wanawake.
Tunaona sisi wenyewe kwenye Umoja wa Mataifa, ambako ninajivunia kuwa tumefikia usawa wa kijinsia kwenye nafasi za juu za uongozi ikiwa ni mara ya kwanza kwenye historia.
Ushahidi uko dhahiri.
Pindi wanawake wanapoongoza serikali, tunaona uwekezaji mkubwa katika hiadhi ya jamii na ukwamukwaji mkubwa dhidi ya umaskini.
Pindi wanawake wanapokuwa kwenye bunge, nchi zinapitisha sera thabiti zaidi za tabianachi.
Pindi wanawake wanapokuwa kwenye meza ya mazungumzo ya amani, makubaliano yanadumu zaidi.
Na sasa wanawake wakiwa ni idadi sawa ya uongozi wa juu kwenye Umoja wa Mataifa, tunaona hatua thabiti zaidi za kusaka amani, maendeleo endelevu na haki za binadamu.
Katika tamaduni zilizokithiri mfumo dume, usawa wa kijinsia unakuwa ni hoja ya madaraka.
Wanaume ni sehemu muhimu katika suluhu.
Natoa wito kwa nchi, kampuni na taasisi kupitisha hatua mahsusi za kusongesha ushiriki sawa wa wanawake na kufanikisha mabadiliko ya haraka.
Tunapojikwamua kutoka kwenye janga, mifumo ya usaidizi inapaswa kulenga wanwake na wasichana, ikiwemo kupitia uwekezaji katika biashara zinazomilikiwa na wanawake na sekta ya malezi.
Kujikwamua kutoka kwenye janga, ni fursa yetu ya kuachana na vizazi vya kuenguliwa na ukosefu wa usawa.
Iwe ni katika kuongoza nchi, biashara au harakati, wanawake wanaleta mchango ambao unalenga maendeleo kwa wote na kuchochea maendeleo ya kufanikisha malengo ya maendeleo endelevu.
Ni wakati wa kujenga mustakabli wa usawa. Hii ni kazi ya kila mt una kwa maslahi ya kila mtu.
Asante.
Open Video Category