Available languages:
António Guterres (Katibu Mkuu) kuhusu Siku ya Kimataifa kwa ajili ya Kutokomeza Ukatili wa Kijinsia dhidi ya Wanawake (25 Novemba 2019)
21 Nov 2019 -  Umoja wa Mataifa umedhamiria kukomesha mifumo yote ya ukatili dhidi ya wanawake na wasichana.
Ukatili huu ni miongoni mwa ukatili mbaya zaidi duniani, unaoendelea na ni ukiukwaji mkubwa kabisa wa haki za binadamu uliosambaa, ukiathiri mtu mmoja miongoni mwa kila wanawake watatu duniani.
Hii inamaanisha mtu mmoja karibu nawe, jamaa wa familia, mfanyakazi mwenzako, rafiki yako au hata wewe mwenyewe.
Ukatili wa kingono dhidi ya wanawake na wasichana chimbuko lake ni karne za mfumo dume.
Hebu tusisahau kwamba pengo la usawa wa kijinsia ambalo limechochea utamaduni wa ubakaji ni suala la kutokuwepo na uwiano wa mamlaka.
Unyanyapaa, dhana potofu, kutoripotiwa vya kutosha na utekelezwaji duni wa sheria, kunachochea ukwepaji wa sheria.
Na ubakaji bado unatumika kama silaha mbaya ya vita.
Yote haya lazima yabadilike sasa.
Natoa wito kwa serikali zote, sekta binafsi, asasi za kiraia na watu kila mahali kuchukua msimamo thabiti dhidi ya dhuluma za kijinsia na ujinga.
Lazima tuonyeshe mshikamano mkubwa na waathirika, watetezi na watetezi wa haki za wanawake.
Na lazima tuchagize haki za wanawake na fursa sawa.
Pamoja, tunaweza na lazima tumalize ubakaji na unyanyasaji wa kijinsia wa kila aina.
Asante
Recent Video On Demand