Available languages:
António Guterres (Katibu Mkuu) Ujumbe siku ya Kimataifa ya Watu Wanaofanya Kazi za Kujitolea 2020
3 Dec 2020 -  Kila mwaka ifikapo tarehe 5 Disemba, dunia huadhimisha siku ya Kimataifa ya watu wanaofanya kazi za kujitolea.
Mwaka huu, tunaangazia mchango wa muhimu wa watu wanaojitolea ili kupambana dhidi ya homa ya mapafu inayosababishwa na virusi vya Corona-19(COVID-19)
Duniai kote, wanaofanya kazi za kujitolea, wamekuwa wakisaidia watu waliodhaifu wakisahihisha taarifa zisizo za kweli, kuelimisha watoto, kutoa mahitaji muhimu kwa wazee, na kuwasaidia wafanyakazi wa afya waliopo mstari wa mbele katika utoaji wa huduma.
Kadri tunavyopata nafuu kutoka kwenye janga hili, wanaofanya kazi za kujitolea watakuwa na jukumu la muhimu la kutekeleza katika kuharakisha dunia inakuwa ya kijani, iliyo jumuishi na yenye uchumi wa haki.
Hakika, wanaofanya kazi za kujitolea ndiyo nguzo kuu kwenye jamii zetu.
Mara kwa mara hufanya kazi na Umoja wa Mataifa, wanaojitolea huleta hali ya kuwa pamoja .
Wanaimarisha Umoja wa jamii
Na wanasaidia kulinda jamii, hasa kwa kuwafikia wale waliopo katika dhiki zaidi.
Hii ndyo sababu, katika Siku ya Kimataifa ya kujitolea, nasihi serikali zote zihamasishe watu kujitolea kufanya kazi, zisaidie jitihada za wanaojitolea na zitambue michango ya watu wanaojitolea ili kuwezesha kufikiwa kwa Malengo ya Maendeleo Endelevu duniani.
Wanaofanya kazi za kujitolea hustahili pongezi za kutoka ndani ya mioyo yetu.
Recent Video On Demand