Available languages:
António Guterres (Katibu Mkuu wa UN) Ujumbe wa Video kwa siku ya usaidizi wa kibinadamu duniani
17 Aug 2018 -  Siku ya usaidizi wa Kibinadamu Duniani ni fursa ya kuonyesha mshikamano na mamilioni ya watu waliokumbwa na vita, migogoro na majanga ya asili.
Familia zinalazimika kuzikimbia nyumba zao kwa ajili ya mustakhbali wasioujua.
Makundi yasiyojiweza, yanalengwa kwa maksudi.
Watoto ambao mustakhbali wao umewekwa njia panda.
Leo, tunawaenzi wahudumu wa misaada ambao huweka maisha yao hatarini kuwasaidia wenye uhitaji. Wao ni ishara ya kweli ya ahadi za kibinadamu. Mashambulizi dhidi ya wahudumu wa misaada yanaendelea kuongezeka.
Hili halikubaliki. Raia wanaokumbwa na vita na wahudumu wa misaada ya kibinadamu sio walengwa.
Tumia sauti yako kwa kampeni yetu.
Hebu tusimame pamoja ili kuokoa maisha na kulinda ubinadamu wetu wa pamoja.
Asante.
Recent Video On Demand