Available languages:
Katibu Mkuu Ujumbe Wa Video Kuhusu Covid-19 Na Taarifa Potofu
14 Apr 2020 -  Wakati dunia ikipambana na janga la mlipuko wa COVID-19, changamoto kubwa kabisa kutukabili tangu Vita Kuu ya pili ya dunia, tunashuhudia pia mlipuko mwingine wa hatari, mlipuko wa taarifa potofu

Duniani kote watu wanaogopa. Wanataka kufahamu cha kufanya na wapi pa kukimbilia kupata ushauri.

Huu ni wakati wa sayansi na mshikamano.

Lakini bado mlipuko wa taarifa potofu unasambaa duniani.

Ushauri wa afya wenye madhara na suluhu zisizo na maana zinaenea.

Uongo ndio unaotawala hewani.

Nadharia potofu zimeghubika na kuathiri mtandao.

Chuki inashika kasi, unyanyapaa na kuwanyanyasa watu na vikundi.

Dunia inapaswa kuungana dhidi ya ugonjwa huu pia.

Na chanjo ni uaminifu.

Kwanza uaminifu katika sayansi.

Nawapongeza waandishi wa habari na wengine ambao wanakagua ukweli wa mlima wa taarifa potofu na machapisho kwenye mitandao ya kijamii.

Kampuni za mitandao ya kijamii zinapaswa kufanya juhudi zaidi kukata mizizi ya chuki na dhana potofu kuhusu COVID-19.

Pili, imani kwa taasisi zinazochukua hatua, wajibikaji, zenye ushahidi na utawala bora na uongozi.Na imani miongoni mwenu.

Kuheshimiana na kudumisha haki za binadamu lazima viwe dira yetu katika kukabilianana mgogoro huu.

Kwa pamoja hebu tuukane uongo na upuuzi uliotawala huko nje.

Leo hii natangaza mkakati mpya wa mawasiliano wa Umoja wa Mataifa ambao utajaza kwenye mtandao taarifa sahihi na sayansi huku ukikabiliana na ongezeko la taarifa potofu, sumu ambayo inayaweka maisha katika hatari zaidi.

Kwa lengo moja la ufahamu na ukweli tunaweza kuishinda COVID-19 na kujenga dunia yenye usawa, haki na mnepo.

Asante
Recent Video On Demand