Available languages:
Katibu Mkuu -- Ujumbe Wa Video Katika Kuadhimisha Mwaka Mpya Wa Kichina
11 Feb 2021 -  Chun Jie Kuai Le! Heei ya mwaka mpya wa kachina!

Natuma salamu zangu za heri kwa kila mtu anayeadhimisha mwaka huu mpya ambao alama yake mwaka huu ni ng’ombe, alama ambayo ni sawa na mwaka wangu wa kuzaliwa. Ng’ombe anaashiria nguvu uthabiti na ujasiri.

Sifa hizo za ng’ombe ni sifa ambazo dunia inahitaji hivi sasa katika kukabiliana na janga la ugonjwa wa Corona au COVID-19.

Mwaka jana janga la COVID-19 limeleta ukosefu mkubwa wa uhakika na mvurugano. Mwaka huu 2021 ni lazima tusimame pamoja kukabili virusi, tuchukue hatua dhidi ya mabadiliko ya tabianchi na tujenge hatua bora za kukwamuka kutoka katika janga.

Naishukuru China na wananchi wa China kwa kuendelea kuunga mkono ushirikiano wa kimataifa na Umoja wa Mataifa katika mihimili yote ya kazi ya chombo hicho chenye wanachama 193.

Natarajia kuendelea kwa ushirikiano wetu. Natuma salamu zangu za heri kwa ajili ya ustawi, afya na furaha kwa mwaka huu wa ng’ombe,

Natuma salamu zangu za heri kwenu nyote za ustawi, afya na furaha katika mwaka huu wa ng’ombe.

Asante sana!
Recent Video On Demand