Available languages:
Ujumbe Wa Katibu Mkuu Wa Umoja Wa Umoja Wa Mataifa Kuhusu Virusi Vya Corona
13 Mar 2020 -  Wapendwa marafiki zahma inayosababishwa na virusi vya Coroka -COVID 19 inatuzunguka sote.
Najua wengi wana hofu, wasiwasi na wamechanganyikiwa.
Hiyo ni hali ya kawaida kabisa.
Tunakabiliwa na tishio lisilo la kawaida la kiafya tofauti na lingine lolote katika wakati wetu
Wakati huohuo virusi vinasambaa, hatari inaongezeka na mifumo yetu ya afya, uchumi na Maisha yetu ya kila siku yako katika majaribu makubwa.
Walio hatarini zaidi ndio wanaoathiriwa Zaidi, hasa wazee wet una wale walio tayari na matatizo ya kiafya, wale wasio na huduma bora za afya na wale walio kwenye umasikini au wanaoishi pembezoni.
Athari za kijamii na kiuchumi kutokana na mchanganyiko wa janga la mlipuko na kudorora kwa uchimi vitatuathiri wengi wetu kwa miezi kadhaa.
Lakini kusambaa kwa virusi kutashika kasi. Uchumi wetu utatengamaa.
Hadi wakati huo lazima tuchukue hatua kwa pamoja ili kupunguza kusambaa kwa virusi na kusaidiana.
Huu ni wakati wa busara na sio kupagawa, sayansi na sio unyanyapaa. Ukweli na si hofu.
Japokuwa hali hii imeelezwa kama janga la kimataifa , ni hali ambayo tunaweza kuidhibiti.
Tunaweza kuzuia kasi ya kusambaa, kuzia maambukizi na kuokoa maisha.
Lakini hiyo itahihaji hatua madhubuti binafsi, za kitaifa na kimataifa.
Tunapaswa kutangaza vita dhidi ya virusi hivi.
Hii inamaanisha nchi zina wajibu wa kujipanga, kuongeza juhudi na kuzidisha hatua.
Kwa kutekeleza mikakati madhubuti ya kuvidhibiti.
Kwa kuzindua na kuboresha mifumo ya kukabiliana na dharura.
Kwa kuongeza kwa kiasi kikubwa uwezo wa upimaji na kuhudumia wagonjwa
Kwa kuweka mazingira bora hospitali, kuhakikisha zina nafasi, vifaa na wahudumu wanaohitajika.
Na kwa kuanzisha hatua za kitabibu za kuokoa maisha.
Nasi sote tuna wajibu wa kutimiza.
Kwa kuzingatia ushauri wa kitabibu na kuchukua hatua. Hatua rahisi za zilizopendekezwa na mamlaka za afya.
Mbali ya kuwa ni mgogoro wa afya ya umma, virusi vinaathiri pia uchumi wa dunia.
Masoko ya fedha duniani yameporomoka vibaya na hali ya sintofahamu.
Mnyororo wa usambazaji duniani umeathirika.
Uwekezaji na mahitaji ya watumiaji vimeathirika huku kukiwa na hatari bayana ya kutumbukia kwenye mdororo wa uchumi ulimwenguni.
Wachumi wa Umoja wa Mataifa wanakadiria kwamba virusi hivyo vinaweza kugharimu uchumi wa ulimwengu angalau dola trilioni 1 mwaka hu una labda zaidi.
Hakuna nchi inayoweza kukabili hili peke yake.
Sasa kuliko wakati mwingine wowote serikali zinapaswa kushirikiana kufufua uchumi , kupanua wigo wa uwekezaji wa umma, kukuza biashara na kuhakikisha msaada unaolengwa kwa watu na jamii zilizoathiriwa zaidi na ugonjwa huu au zilizo katika hatari zaidi ya athari mbaya za kiuchumi wakiwemo wanawake ambao mara nyingi hubeba mzigo mkubwa wa kazi ngumu ya kutoa huduma.
Wapendwa janga hili linarejesha nyumbani umoja wetu ambao ni muhimu katika familia ya ubinadamu wetu.
Kuzuia kuenea zaidi kwa COVID-19 ni jukumu letu zote kwa pamoja.
Umoja wa Mataifa likiwemo shirika la afya duniani umejipanga kikamilifu.
Kama sehemu ya familia yetu ya kibinadamu tunafanya kazi saa 24 siku 7 kwa wiki na serikali ili kutoa muongozo wa kimataifa kuusaidia ulimwengu kuchukua hatua za kukabili tishio hili.
Tuko pamoja nawe katika mshikamano huu.
Tuko pamoja katika hili, na tutalikabili hili kwa pamoja
Asante
Recent Video On Demand