Available languages:
António Guterres (Katibu Mkuu) Ujumbe wa video wa Siku ya Haki za Binadamu (10 Desemba 2019)
10 Dec 2019 -  Mwaka huu, katika
Siku ya Haki za Binadamu, tunasherehekea jukumu la vijana katika kuhuisha haki za binadamu.
Ulimwenguni kote , vijana wanaandamana, kuandaa, na kupaza sauti:
Kwa haki ya mazingira yenye afya …
Kwa haki sawa kwa wanawake na wasichana…
Kushiriki katika kufanya maamuzi …
Na kutoa maoni yao kwa uhuru…
Wanaandamana kwa ajili ya haki yao ya mustakabali wa amani, haki na fursa sawa.
Kila mtu ana haki ya haki zote: za kiraia, kisiasa, kiuchumi, kijamii na kitamaduni. Bila kujali wanaishi wapi. Bila kujali wapi wanaishi, kabila, dini, asili yao, jinsia, mwelekeo wa kijinsia, kisiasa au maoni mengine, ulemavu au kipato, au hali yoyote ile.
Katika Siku hii ya Kimataifa, nataka kila mtu awasaidie na kuwalinda vijana ambao wanasimama kwa ajili ya haki za binadamu.
Open Video Category