Available languages:
António Guterres (Katibu Mkuu) wa aadhimisho ya miaka 30 ya Baraza la Haki za Mtoto (20 Novemba 2019)
18 Nov 2019 -  Miaka 30 iliyopita, mataifa yalikusanyika kutoa ahadi kwa watoto duniani.
Kwa mara ya kwanza, Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Mtoto ulieleza bayana haki za msingi za mtoto wa kike na wa kiume.
Nchi zote zilitambua hali ya hatari ya kipekee inayokabili watoto na kuahidi kuwapatia chakula, huduma ya afya, elimu na ulinzi.
Tangu wakati huo, kumekuwa na maendeleo.
Idadi ya vifo vya watoto imepungua kwa zaidi ya nusu na udumavu wa watoto ulimwenguni umepungua.
Lakini mamilioni ya watoto bado wanakabiliwa na vita, umaskini, ubaguzi na magonjwa.
Ulimwenguni kote, watoto wanatuonyesha uthabiti na uongozi wao wakichechemua ulimwengu endelevu zaidi kwa wote.
Tunapoadhimisha miaka 30 ya mkataba huu muhimu, nasihi nchi zote zitime ahadi zao.
Tusongeshe maendeleo tuliyofikia na tuahidi kujali watoto kwanza.
Kila haki kwa kila mtoto.