Available languages:
Nafasi ya wanawake ni muhimu katika sitisho la mapigano duniani
1 Jun 2020 -  Wasaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu masuala ya Wanawake, Siasa na Ujenzi wa amani na Operesheni za Ulinzi wa Amani, wanatoa wito wa pamoja kuhakikisha wanawake ndio kitovu cha juhudi za sitisho la mapigano duniani. Wanasema kuwa janga la COVID-19 duniani, ni kengele ya dharura: dunia haiwezi kukabili mapigano na wakati huo huo janga la ugonjwa. Hii ndio maana wito wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa sitisho la mapigano ulimwenguni ni muhimu sana. Wanawake kila mahali wanafanya kazi dhidi ya nadharia za ajabu ili kuleta amani. Wanawake wakishiriki kikamilifu, tutaibuka washindi katika janga hili.