Available languages:
KATIBU MKUU UJUMBE WA VIDEO KWA AJILI YA SIKU YA MAZINGIRA DUNIANI (2019)
5 Jun 2019 -  Siku ya mazingira duniani inatanabaisha ni jinsi gani sote tunavyotegemea mali asili kwa ajili ya afya ya sayari yetu.
Ubora wa maji tunayokunywa, chakula tunachokula na hewa tunayovuta vyote vinategemea uhifadhi wa maliasili duniani.
Lakini mazingira yanakabiliwa na changamoto kubwa zinazosababishwa na shughuli za binadamu.
Aina milioni moja za viumbe viko hatarini kutoweka. Bahari ziko katika shinikizo kubwa.
Uchafuzi wa hewa unakatili maisha ya watu milioni saba kila mwaka na kuathiri ukuaji wa watoto. Wachafuzi wengi wa hewa pia husababisha ongezeko la joto duniani.
Na mabadiliko ya tabianchi ni tishio kubwa.
Katika ziara yangu ya hivi karibuni Pasifiki ya Kusini nimeshuhudia athari kubwa na mbaya zaidi za dharura ya hali ya hewa duniani.
Hakuna muda wa kupoteza. Hivi ni vita vya maisha yetu.
Ni lazima tushinde. Na tunaweza. Suluhu zipo.
Toza kodi uchafuzi, sio watu.
Acha kufadhili mafuta yanayochimbwa.
Acha kujenga mitambo mipya ya makaa ya mawe.
Watu kila mahali wanadai hatua zichukuliwe.
Siku ya Mazingira Duniani, hebu tuutii wito wao.