Available languages:
Ujumbe wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika maadhimisho ya Siku ya Walinzi wa Amani Duniani 2020
27 May 2020 -  Leo hii tunawatunuku zaidi ya wanaume na wanawake milioni moja na zaidi ambao wamejitolea kufanya kazi ya ulinzi wa amani wa Umoja wa Mataifa pamoja na zaidi ya watu 3,900 ambao wamepoteza maisha yao wakati wakitekeleza majukumu yao.
Pia tunawashukuru zaidi ya raia 95,000, watumishi kutoka polisi na jeshi wanaofanya kazi hizo duniani kote.
Wanakabiliwa na mojawapo ya changamoto kubwa zaidi ya kujitolea kwenye majukumu yao ya kulinda amani wakati huohuo wakishughulikia changamoto za baa la virusi vya COVID-19.
Kauli mbiu ya maadhimisho ya mwaka huu-Wanawake na Ulinzi wa Amani- unaainisha umuhimu wao wa kipekee katika shughuli zetu za kulinda amani.
Wanawake kwa kawaida huwa na nafasi kubwa zaidi ya kufikia jamii tunazozitumikia, hali hii hutuwezesha kuboresha ulinzi wa raia, kuendeleza haki za binaadamu na kuboresha utekelezaji kwa ujumla.
Hii ina umuhimu zaidi wakati huu, ambapo walinzi wa amani wanawake wako mstari wa mbele kusaidia mwitikio wa kushughulikia COVID-19 katika jamii ambazo tayari ni hafifu-kwa kutumia redio jamii kueneza jumbe zinazohusu afya ya umma, kwa kuwasilisha mahitaji maalumu kwa jamii ili wajizatiti, na kusaidia jitihada za wajenga amani ambao ni raia. Hata hivyo, wanawake wanaendelea kuwasilisha asimia 6 tu ya wanajeshi na polisi wanaovaa magwanda, watumishi wa utawala wa sheria na maafisa warekebishaji wanaofanya kazi kwenye Ulinzi wa Amani.
Wakati tukiadhimisha miaka 20 ya Azimio la Baraza la Usalama lenye kumbukumbu ya 1325 linalohusu Wanawake, Amani na Ulinzi, tunapaswa tufanye zaidi kufikia usawa wa uwakilishi wa wanawake katika nyanja za amani na ulinzi.
Pamoja, tuendeleze jitihada za kuleta amani, kushinda baa hili na kujenga maisha bora ya baadae.