Available languages:
Ujumbe Wa Video Wa Siku Ya Kimataifa Ya Kumbukizi Ya Waathirika Wa Utumwa Na Biashara Ya Utumwa Ya Kuvuka Atlantiki 2019
18 Mar 2019 -  Biashara ya utumwa iliyohusisha kuvushwa bahari ya Atlantiki, ilikuwa ni kitu cha kuchukiza zaidi katika mlolongo wa matukio ya ukatili dhidi ya binadamu.
Katu hatupaswi kusahau uhalifu huu na madhara yake barani Afrika na kwingineko karne na karne.
Mradi wa Umoja wa Mataifa wa kumbukizi ya utumwa, unasaidia kuhakikisha kuwa mafunzo yanaeleweka na yanasikika hata hii leo.
Watumwa walihangaika dhidi ya mfumo wa sheria ambao walifahamu haukuwa sawa.
Katika matukio mengi, waliweka rehani maisha yao wakiwa na matumaini ya kuwa huru.
Tunapaswa kuelezea simulizi za wale waliosimama kidete dhidi ya wakandamizaji wao, na kutambua haki yao sahihi ya kupinga.
Katika siku hii ya kimataifa ya kumbukizi ya waathirika wa utumwa, tunakumbuka mamilioni ya wanaume, wanawake na watoto wa kiafrika ambao walinyimwa ubinadamu wao na kulazimishwa kuhimili ukatili wa kutisha.
Tunawaenzi kwa kusimama kidete dhidi ya aina zote za sasa za utumwa, kwa kuelimisha juu ya hatari za ubaguzi wa sasa, na kwa kuhakikisha kuwa haki na fursa sawa leo hii kwa watu wote wenye asili ya Afrika.
Asanteni.