Available languages:
António Guterres (Katibu Mkuu) kuhusu Siku ya Umoja wa Mataifa (24 Oktoba 2019)
18 Oct 2019 -  Ujumbe wa video wa António Guterres, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, kuhusu siku ya Umoja wa Mataifa.
Siku ya Umoja wa Mataifa inaangazia malengo makuu ya Mkataba wa Umoja wa Mataifa uliopitishwa siku kama hii miaka 74 iliyopita.
Licha ya hali ya changamoto kubwa tulizo nazo, Mkataba huo unabaki kuwa nanga yetu ya maadili ya pamoja.
Wakati huu wa mabadiliko mengi sana, Umoja wa Mataifa umejikita katika kuangazia matatizo halisi ya watu halisi.
Tunafanya bidii ili kuwa na usawa katika utandawazi na hatua dhidi ya mabadiliko ya tabianchi.
Tunapigania haki za binadamu na usawa wa kijinsia - na kusema "hapana" kwa chuki ya aina yoyote.
Na tunajitahidi kudumisha amani – huku tukitoa msaada wa kuokoa maisha kwa milioni ya watu wanaoathirkia na vita vya silaha.
Shirika la Umoja wa Mataifa lenyewe linazidi kuwa thabiti na kuwajibika tunapoendelea kuongeza msaada kwa nchi.
Mwaka ujao tunaadhimisha miaka 75 ya Shirika hili. Maadhimisho haya ya kihistoria ni wakati muhimu wa kujenga mustakabali wetu, kwa pamoja.
Ninakualika ujiunge katika mazungumzo haya.
Pamoja, hebu tuendeleze ustawi wetu sisi binadamu.
Shukrani.