Available languages:
António Guterres (Katibu Mkuu wa UN) kuhusu Muongo wa Hatua kwa ajili ya Malengo ya Maendeleo Endelevu
12 Mar 2020 -  Ujumbe wa video wa António Guterres, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Muongo wa Maendeleo Endelevu.
Malengo ya maendeleo endelevu ni mpango wa hatua wa dunia kwa ajili ya usawa wa utandawazi na mustakabali bora kwa wote.
Tuna miaka kumi ya kutimiza ndoto hiyo na tunaweza kufikia hapo tu kwa pamoja.
Ndio sababu tumezindua muongo wa hatua ili kutimiza malengo hayo.
Kuushinda umasikini na pengo la usawa.
Kukabiliana na mgogoro wa mabadiliko ya tabianchi na kusongesha usawa wa kijinsia.
Kujenga jamii zenye amani, haki na jumuishi, zilizo huru dhidi ya ubaguzi na chuki, zinazojali mazingira.
Jiunge nasi.
  Chukua hatua.
  Tumia fursa hii.
  Hebu tufanye kazi kwa pamoja ili kufikia Malengo, kusongesha mbele ulimwengu wetu na tusimwache mtu yeyote nyuma.
  Asante.