Available languages:
Javier Perez de Cuéllar, 1920-2020
4 Mar 2020 -  Javier Pérez de Cuéllar, ambaye alikuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika muongo ulioshuhudia misukosuko kuanzia mwaka 1982, ameacha mchango wa amani duniani kote kutokana na juhudi zake za kuimarisha mazungumzo, kuleta pande kinzani pamoja na kufanisha usuluhishi. Katibu Mkuu huyu wa kwanza wa UN kutoka nchi za Amerika ya Kusini alishikilia maadili ya Umoja wa Mataifa hata baada ya kumaliza kipindi chake cha uongozi, akichechemua amani, haki, haki za binadamu na utu wa binadamu wakati wote wa uhai wake.