Available languages:
Katibu Mkuu -Ujumbe Wa Video Kwa Ajili Ya Siku Ya Kimataifa Ya Kupunguza Hatari Za Majanga (13 octoba 2019)
10 Oct 2019 -  Katika maisha yangu yote nimezuru jamii nyingi zilizoathiriwa na matukio mabaya ya hali ya hewa na majanga mengine ya asili.
Kuanzia Pasifiki Kusini hadi Msumbiji, mpaka Caribbea na zaidi, nimejionea uharibifu na athari zilizobadili maisha kutokana na dharura ya mabadiliko ya tabianchi kwa jamii zisizojiweza.
Majanga yanasababisha madhara makubwa na yanaweza kwa muda mfupi kufuta miongo ya maendeleo yaliyopatikana.
Katika muongo ujao dunia itawekeza matrilioni ya dola katika makazi mapya, shule, hospitali na miundombinu. Mnepo dhidi ya tabianchi na upunguzaji wa hatari ya majanga ni lazima viwe kiini cha uwekezaji huu.
Kuna sula la msingi la kiuchumi kwa hatua kama hizo: kufanya miundombinu kuwa na mnepo zaidi dhidi ya tabianchi kunaweza kuwa na faida za uwiano wa sita kwa moja. Kwa kila dola inayowekezwa, dola sita zinaweza kuokolewa.