Available languages:
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa - Ujumbe wa Video kwa Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani
1 May 2019 -  Ujumbe wa Video kwa Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani.
Vyombo huru vya habari ni muhimu kwa amani, haki na haki za binadamu kwa wote.
Ni muhimu kujenga jumuiya za uwazi na za kidemokrasia na kuwawajibisha wale walio madarakani.
Ni muhimu kwa maendeleo endelevu.
Waandishi wa habari na wafanyakazi wa vyombo vya habari hutanabaisha kuhusu changamoto za ndani na za kimataifa na kueleza taarifa zinazohitaji kuelezwa.
Huduma yao kwa umma ni ya thamani kubwa.
Sheria ambazo zinalinda uandishi huru wa habari, uhuru wa kujieleza na haki ya kupata habari zinahitajika kupitishwa, kutekelezwa na kuhakikishwa.
Uhalifu dhidi ya waandishi wa habari lazima uchukuliwe hatua za kisheria.
Katika Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani 2018, Natoa wito kwa serikali kuimarisha uhuru wa vyombo vya habari na kuwalinda waandishi wa habari.
Kuchagiza vyombo huru vya habari ni kusimamia haki yetu ya kupata ukweli.
Asanteni.