Available languages:
Ujumbe Wa Katibu Mkuu Wa Umoja Wa Mataifa Kuhusu Siku Ya Chakula Duniani (16 oktoba 2019)
11 Oct 2019 -  Siku ya chakula duniani ni wito kwa ajili ya kutokomeza njaa- na kuwa na dunia ambako chakula chenye lishe bora kinapatikana kwa bei nafuu na kwa watu wote na kila mahali.
Lakini hii leo, zaidi ya watu milioni 820 hawana chakula cha kutosheleza mahitaji yao.
Na dharura ya mabadiliko ya tabianchi ni tishio kwa uhakika wa chakula.
Wakati huo huo, watu bilioni mbili, wanaume, wanawake na watoto wana uzito kupita kiasi au ni matipwatipwa.
Milo isiyo bora inazua hatari ya magonjwa na vifo.
Haikubaliki kwamba njaa inaongezeka wakati ambako dunia inatupa takriban tani bilioni moja ya chakula kila mwaka.
Ni wakati wa kubadilisha namna ambavyo tunazalisha, tunatumia, ikiwemo kupunguza gesi chafuzi.
Kubadilisha mifumo ya chakula ni muhimu katika kufanikisha malengo ya maendeleo endelevu.
Ndio sababu ninatarajia kuandaa kongamano la mifumo ya chakula mwaka 2021 kama sehemu ya muongo wa hatua kufanikisha malengo ya maendeleo endelevu.
Kama familia ya binadamu, dunia isiyo na njaa ni wajibu wetu.