Available languages:
Katibu Mkuu Ujumbe Wa Video Kwa Ajili Ya Siku Ya Radio Duniani
13 Feb 2020 -  Radio inawaleta watu pamoja. Katika enzi za mageuzi ya haraka ya vyombo vya Habari, Radio inakuwa ni sehemu maalum katika kila jamii kama chanzo cha cha Habari muhimu na taarifa.
Lakini radio pia ni chanzo cha uvumbuzi ambao uliendeleza mazungumzo na wasikilizaji na taarifa zilizotokana na watumiaji wa chombo hicho kwa miongo kadhaa kabla ya kuwa maarufu.
Redio inatoa taswira nzuri ya utofauti katika mundo wake, lugha zake, na miongoni mwa wataalam wenyewe wa redio.
Hii inatuma ujumbe muhimu kwa dunia. Tunapojitahidi kufikia malengo ya maendeleo endelevu na kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi radio inajukumu muhimu la kufanya kama chanzo cha habari na mchagizaji.
Katika siku hii ya Radio Duniani hebu tutambue uwezo wa radio katika kuchagiza utofauti na kusaidia kujenga dunia ya amani na jumuishi.