Available languages:
Ujumbe wa video wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres kuhusu siku ya utu wa bindamu 2017
18 Aug 2017 -  Ujumbe wa video wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres, kuhusu vijana juu ya siku ya utu wa bindamu 2017.
Leo, mamilioni ya watu kote duniani wameghubikwa na mizozo ambayo hawakuianzisha.
Wanawake, wasichana, wanaume na wavulana wa kawaida wamejikuta katikati ya vita au kulengwa moja kwa moja na machafuko, yakiwalazimisha mamilioni kuzikimbia nyumba zao na kukabiliwa na sintofahamu ya mustakhbali wao.
Kufuatia mateso na ukosefu wa haki, wafanyakazi wa afya wenye ujasiri na wahudumu wa misaada ambao wamejitolea kusaidia mara kwa mara wanakabiliwa na mashambulizi mabaya ambayo huzuia uwezo wao wa kuokoa maisha.
Mwaka huu Umoja wa Mataifa na washirika wetu tunaadhimisha siku ya huduma za kibinadamu duniani kwa wito wa kuwalinda raia waliojikuta katikati ya vita na wafanyakazi wa afya na huduma za kibinadamu wanaowasaidia.
Tunataka dunia itambue: :raia, wakiwemo wahudumu wa misaada na wafanyakazi wa afya , sio walengwa.
Tafadhali shikamana na raia kwa kupaza sauti yako kwenye kampeni yetu. Kila mtu anaweza kuleta mabadiliko katika kumaliza vurugu na kuzingatia maadili tunayoshiriki na kuyadumisha.
Asante.
(World Humanitarian Day 2017, #WorldHumanitarianDay)