Available languages:
Katibu-Mkuu Ujumbe Wa Siku Ya Kimataifa Ya Vijana
8 Aug 2019 -  Siku ya Kimataifa ya Vijana imeadhimishwa kwa miaka 20 sasa. Mwaka huu, siku ya Vijana inajikita na mada ya mabadiliko katika elimu ili kuifanya iwe jumuishi zaidi, rahisi kupatikana na inayokwenda na dunia ya sasa.

Tunakabiliwa na mgogoro wa kujifunza. Mara nyingi shule haziwawezeshi vijana kupata ujuzi wanaouhitaji kwenda sanjari na mapinduzi ya teknolojia. Wanafunzi wanachokihitaji sio kusoma tu, lakini pia kusoma jinsi ya kujifunza.

Elimu ya sasa inapaswa kuchanganya maarifa, stadi za maisha na fikra. Inapaswa kujumuisha habari kuhusu uendelevu na mabadiliko ya tabianchi. Na inapaswa kuendeleza usawa wa kijinsia, haki za binadamu na utamaduni wa amani.

Vitu hivi vyote vimejumuishwa katika Vijana 2030, mkakati wa Umoja wa Mataifa wa kuongeza ushiriki wetu na vijana na kuwaunga mkono katika kufikia haki zao.

Leo tunawasherehekea vijana, mashirika yanayoongozwa na vijana, serikali na wengineo ambao wanafanya kazi ili kubadili elimu na kuwainua vijana kila mahali.
Recent Video On Demand