Available languages:
Ujumbe Wa Katibu Mkuu Wa Umoja Wa Mataifa Katika Kuadhimisha Kumbukumbu Ya Mauaji Ya Kimbari Dhidi Ya Watutsi Nchini Rwanda
6 Apr 2020 -  Leo, tunakumbuka mauaji ya kimbari dhidi ya watutsi nchini Rwanda---wakati watu zaidi ya milioni moja, waliuawa kwa utaratibu ndani ya siku 100.

Waathirika walikuwa watutsi, lakini pia ilihusisha wahutu na wengine ambao waliyapinga mauaji ya kimbari.

Katika siku hii, tunawaenzi wale waliouawa.

Na tunapata msukumo kutoka kwenye uwezo wa wale ambao walinusurika kwa kuwa na maridhiano na urejeaji katika maisha ya kawaida.

Hatupaswi kamwe kuruhusu ukatili kama huo kutokea tena.

Tunapaswa kusema hapana dhidi ya kauli za chuki na ubaguzi, na kukataa kujitenga, utaifa na uwekaji wa mipaka.

Ni kwa kutambua tu kwamba sisi sote ni familia moja ya wanadamu ndani ya sayari moja ndipo tutaweza kuzimudu changamoto nyingi za ulimwengu ambazo zinatukabili - kutoka kwa COVID-19 hadi mabadiliko ya tabianchi.

Tangu mauaji ya kimbari, Rwanda imeonesha kuwa inawezekana kunyanyuka kutoka katika majivu, kupona na kujenga upya jamii imara na iliyoendelevu zaidi.

Tunapoangalia mbele kuongeza kasi ya juhudi za kufanikisha Malengo ya Maendeleo Endelevu, wacha tuchukue funzo kutoka katika somo linaloendelea la Rwanda.
Recent Video On Demand