Available languages:
KATIBU MKUU UJUMBE WA VIDEO KWA AJILI YA SIKU YA WAKIMBIZI DUNIANI (20 Juni 2019)
19 Jun 2019 -  Katika siku ya wakimbizi duniani fikra zangu ziko na wanawake, wanaume na Watoto Zaidi ya milioni 70, wakimbizi na wakimbizi wa ndani ambao wamelazimika kukimbia vira, migogoro na mateso.

Hii ni idadi kuwa ya kushangaza -mara mbili ya ilivyokuwa mika 20 iliyopita.

Watu wengi waliolazimika kutawanywa wanatoka katika baadhi tu ya nchi : Syria, Afghanistan, Sudan Kusini, Myanmar na Somalia.

Katika miezi 18 iliyopita mamilioni Zaidi wamekimbia Venezuela.

Napenda kutambua utu wa nchi ambazo zinahifadhi wakimbizi hata kama zenyewe zinakabiliwa na changamoto za kiuchumi na matatizo ya kiusalama.

Tunapaswa kuenzi ukarimu wao kwa maendeleo na uwekezaji.

Inasikitisha kwamba mfano wao haufuatwi na wote .

Tunapaswa kufufua upya uaminifu wa utawala wa ulinzi wa kimataifa.

Mkataba wa kimataifa wa wakimbizi uliopitishwa Disemba mwaka jana unatoa mwongozo wa hatua za kisasa za kuchukua kuhusu wakimbizi.

Wakimbizi wanachokitaka Zaidi ni amani.

Mamilioni ya watu kote duniani wamejiunga na kampeni ya UNHCR ya siku ya wakimbizi duniani na kuchukua hatua ziwe kubwa au ndogo kushikamana na wakimbizi.

Waweza kuchukua hatua kushikamana na wakimbizi pia?

Asante