Available languages:
UJUMBE WA KATIBU MKUU KWA AJILI YA SIKU YA KIMATAIFA YA VIJANA
11 Aug 2017 -  Habari kila mmoja,!
Nina furaha kuwahutubia katika siku ya kimataifa ya vijana.
Kama Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nimejidhatiti katika kuwawezesha vijana na kumjumisha kila kijana kote duniani.
Kwa mtazamo huu , nimemteua mwakilishi maalamu mpya wa vijana Jayathma Wickramanayake.
Ni mjumbe mgogo kabisa katika timu yangu na muhimu sana.
MWAKILISHI WA VIJANA: Kizazi cha leo cha vijana ndio kikubwa kabisa katika historia. Hivi sasa tuko bilioni 1.8 katika duniani hii ambayo ina fursa nzuri , lakini pia changamoto.
Leo hii, vijana milioni 73 hawana ajira. Zaidi ya vijana milioni 600 wanaishi katika hali tete au katika mazingira yaliyoathiriwa na vita. Na zaidi ya vijana milioni 400 hawana fursa ya huduma muhimu za afya.
Hili lazima libadilike.
Tumejidhatiti kufanya nao kazi kwa bidi na kwa ajili ya vijana kutambua na kudimisha haki zao, na kuchagiza uraia wao wa kimataifa. Na hilo ndilo niko hapa kulifanya.
MWAKILISHI WA VIJANA: Jumuika nasi katika kuchagiza vijana!
KM: Pamoja tunaweza kujenga dunia yenye amani kwa vizazi vijavyo.
KM na MWAKILISHIWAVIJANA: Asante!

(2017 International Youth Day)
Open Video Category