Available languages:
Ndani ya uwezo wetu
20 Apr 2021 -  Aidan Gallagher, mwigizaji, mwimbaji na balozi mwema wa shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa mazingira duniani, UNEP anaeleza jinsi gani mkataba wa Paris wa mabadiliko ya tabianchi ndio njia ya kuunda dunia yenye hewa safi na nishati safi yenye misitu na bahari bora. Tunapokaribia Siku ya Sayari Dunia na mkutano wa viongozi wa mabadiliko ya tabianchi, hatua za pamoja za kudhibiti ongezeko la joto duniani ni dharura kuliko wakati mwingine wowote. Hii ni video ya kwanza katika mlululizo uitwao Ndani ya uwezo wetu. Ikiwa imekaririwa na wanamazingira kutoka kote duniani , Ndani ya uwezo wetu, inaonesha jinsi gani mkataba wa mabadiliko ya tabianchi utakavyosaidia kutatua mgogoro wa mabadiliko ya tabianchi. #HatuazaMabadilikoyatabianchi #ClimateAction